27 Januari 2023 - 15:10
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Ulimwengu wa Magharibi una wasiwasi kuhusu mvuto wa Uislamu

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema: "Ulimwengu wa makafiri unauogopa Uislamu, na ulimwengu wa Magharibi una wasiwasi kuhusu mvuto wa Uislamu."

Hujjat-ul-Islam wa Muslimin Kazem Siddiqui, imamu wa muda wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran katika khutba zake ameashiria vitendo vya hivi karibuni vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na kusema kuwa, ulimwengu wa makafiri unauogopa Uislamu na ulimwengu wa Magharibi una wasiwasi juu ya mvuto wa Uislamu.

Hujjat-ul-Islam wa Muslimin Kazem Siddiqui, amegusia pia vikwazo vya Wamagharibi dhidi ya Iran na kusema moja ya taasisi zilizolengwa ni Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC). Ameongeza kuwa, jeshi hilo limejitolea kwa ajili ya dini, mapinduzi, watu na nchi tangu kuasisiwa kwake.

Khatibu Sala ya Ijumaa aliongeza kuwa: "IRGC pia imehudumia watu wa Ulaya kwa sababu Luteni Jenerali Shahidi Qassem Soleimani, kwa ubunifu wake na  kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, aliweza kuunda harakati ya Mujahidina na kupigana na  kundi la kigaidi la Daesh au ISIS, ambalo liliundwa na nchi za Ulaya na Marekani, na hivyo IRGC ilizuia moto wa Daesh kufika Ulaya."

Halikadhalika amesema madola ya Magharibi yanataka  IRGC iwe dhaifu, lakini IRGC itaimarika zaidi na madola hayo yatafedheheka.

342/